Thursday, October 18, 2012

ASKARI MKOANI RUKWA WANATARAJIWA KUPATA MAFUNZO YA TEHAMA.




ASKARI wa jeshi la polisi mkoani Rukwa wanarajiwa kuendelezwa kielimu kupitiya Chuwo Kikuu Huriya Cha Tanzaniya kituwo cha Rukwa, ili wawe weledi katika taaluma ya Teknolojiya ya Habari na Mawasiliano kwa njiya ya mtandawo, hayo yalielezwa na kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda alipotembelewa na Wandishi wa Habari ofisini kwake baada ya mafunzo ya uandishi wa habari kwa njiya ya mtandawo mwaka huu, oktoba 18. Picha, Na; Franco Nkyandwale sumbawanga.

MIUNDO MBINU SHULENI SI RAFIKI KWA WALEMAVU.

Mwanafunzi wa darasa la Tatu Atupele Sanga wa Shule moja ya Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, akisaidiwa na rafiki zake kuingiya darasani, kwani miundo mbinu ya shule yake si rafiki. Picha Na; Franco Nkyandwale Sumbawanga.

MAZOEZI HUJENGA UMAKINI WA KAZI

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa Habari kwa njiya ya mtandao wa RUKWA PRESS CLUB katika siku ya tatu kati ya siku nne wakifanya mazoezi kwa vitendo wakiwa na Mwezeshaji Lukelo Mkami  aliyesimama kushoto katika Ukumbi wa Chama Cha Walimu Sumbawanga, Oktoba 18, Mwaka huu.

Wednesday, October 17, 2012

YA KALE DHAHABU

ASILI: Baadhi ya wakazi wa Kyela mkoani Mbeya asili yao ni wakisi hutumia vyungu kama hivi katika matumizi ya vyombo vya nyumbani, hiki ni sawa na Kipozeo cha maji,  Friza.PICHA KUTOKA MTANDAO WA GOOGLE.